DAR ES SALAAM:MWANAMITINDO na ‘video queen’ Fatma Khamis ‘Fayvanny’ ameweka wazi kutokutaka kwake tena kuwasiliana na mzazi mwenzake, msanii Raymond Shabani ‘Rayvanny’, na kusema hakuna haja ya kurudiana.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Fayvanny ameweka ujumbe mkali akielezea hisia zake kwa Rayvanny na kumwambia aache kumtafutia maelezo au kumlazimisha kurejea mahusiano yao.Katika ujumbe huo ameandika miongoni mwa mengine:

“Umekaa upo busy kunitafutia sababu unataka tuwe na mzani sawa, wewe una matendo hadi shetani anakuogopa.
Nikisema niyaweke matendo yako hapa duniani itakushangaa; hakuna mtu anaweza kukusogelea maana wewe sio binadamu wa kawaida. Wewe niache, usinitafute kwani lazima kuwa na mimi si utafute wengine.
Achana na mimi maana vita yangu hutoiweza; ushukuru tu nakupa heshima kidogo na na kuhifadhi kwa sababu ya hiki kiumbe, basi bila hivyo ungejuta.”
Spoti Leo imemtafuta Rayvanny ili akutane nao na kumweleza suala hili lakini simu zake hazikupokelewa.Tunaendelea kumtafuta msanii huyo ili kupata upande wake na kujua kama kuna njia ya kutatua tofauti zao, hasa kwa kuwa wote ni wazazi.
The post Fayvanny amkataa Rayvanny first appeared on SpotiLEO.




