SHOMARI Kapombe beki wa Simba SC amebainisha kuwa watajitoa kwa nguvu zote kuzuia makosa kwenye mchezo dhidi ya Yanga SC ili wasifungwe.
Mchezo wa funga kazi msimu wa 2024/25 kwa wababe hawa wawili ulichezwa Juni 25 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC, mabao ya Pacome na Mzize yaliwapa pointi tatu Yanga SC.
Leo Septemba 16 2025 unakwenda kuchezwa mchezo wa kwanza ikiwa ni kufungua pazi la Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/26 inayotarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025 na mabingwa watetezi wakiwa ni Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Romain Folz.
Yanga SC na Simba SC zinatarajiwa kukutana leo Uwanja wa Mkaka kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ikiwa ni ufunguzi wa msimu mpya wa 2025/26.