LONDON: MCHEZAJI wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ghana Thomas Partey amekana mashataka matano yanayomkabili ya kuwabaka wanawake wawili na kumdhalilisha kingono mwanamke mwingine mmoja.
Kiungo huyo mchachari wa Villareal amekana mashtaka hayo matano ya ubakaji na shtaka moja la unyanyasaji wa kingono alipofika katika Mahakama ya Southwark Crown jijini London leo Septemba 17.
Makosa hayo yanadaiwa kufanyika kati ya mwaka 2021 na 2022, wakati mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 akiichezea Arsenal kwenye Premier League. Alishtakiwa siku nne baada ya kuondoka katika klabu hiyo ya kaskazini mwa London, kufuatia kumalizika kwa mkataba wake mwishoni mwa mwezi Juni.
Partey yupo nje kwa dhamana hadi kesi hiyo ya ubakaji itakapotajwa tena tarehe 2 Novemba mwaka ujao. Masharti ya dhamana hiyo hayamzuii kucheza soka, lakini ni lazima awajulishe polisi juu ya safari yoyote ya kimataifa saa 24 kabla na asiwasiliane na walalamikaji hao kwa namna yeyote.
Kiungo huyo ambaye sasa anachezea klabu ya Villareal ya Hispania, tayari alikuwa nchini England wakati timu yake mpya ilipocheza na Tottenham hotspurs kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Aliingia kama mchezaji wa akiba katika mchezo waliopoteza kwa bao 1-0.
The post Partey akana mashataka ya ubakaji first appeared on SpotiLEO.