PARIS: WINGA wa kushoto wa mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Paris Saint-Germain Khvicha Kvaratskhelia amepona kwa wakati jeraha la mguu tayari kujumuishwa kwenye kikosi cha PSG kikianza kutetea ubingwa wake dhidi ya Atalanta usiku wa leo Jumatano.
Winga huyo alipata jeraha Jumapili wakati kikosi hicho kikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Lens kwenye Ligue 1 ya Ufaransa na kuzua shaka kwa mechi hii ya katikati wiki dimbani Parc des Princes.
Lee Kang-in, ambaye alilazimika kutoka uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Lens, pia amerejea kwenye kikosi cha kocha Luis Enrique.
PSG, ambayo imeendeleza msimu wake mzuri wa Ligue 1 kwa ushindi wa nne mfululizo, itawakosa washambuliaji wake Ousmane Dembélé na Désiré Doué kutokana na majeraha. Beki wa Mbrazil Lucas Beraldo pia atakosekana baada ya kuteguka kifundo cha mguu wake wa kushoto.
The post PSG kamili kuivaa Atalanta first appeared on SpotiLEO.