DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Hip Hop, Rosary Roberth ‘Rose Ree’, ametangaza kuingia kwenye mfungo maalum kwa ajili ya kuliombea taifa la Tanzania, akiwahimiza mashabiki wake kushiriki naye katika sala hizo.
“Natangaza siku tatu za maombi ya kufunga, kusali na kujinyima. Wiki hii tule mboga mboga na matunda pekee, kisha wiki ijayo Jumatatu, Jumanne na Jumatano (tarehe 22, 23 na 24) tufunge mfululizo,” ameandika msanii huyo.
Ameongeza kuwa maombi hayo ni maalum kwa ajili ya kuiombea Tanzania iendelee kudumu katika amani, mshikamano na mshikamano wa kitaifa.
“Wengi walitangulia mbele yetu kupigania haki, uhuru na amani. Ni jukumu letu kuhakikisha vinadumu, damu na jasho lao havikumwagika bure,”
Rosa Ree amewataka mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kushiriki katika mfungo huo, akisema ni “prayers up for Tanzania.”amemalizia.
The post Rosa Ree atangaza siku tatu za maombi ya kuliombea taifa first appeared on SpotiLEO.