DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu nchini, Rose Ndauka, ameteka hisia za mashabiki wake baada ya kuoneesha kuwa bado anawathamini na kutambua mchango wao mkubwa katika safari yake ya kisanaa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rose ameandika kuwa mafanikio aliyofikia yametokana na nguvu na sapoti ya jamii inayomzunguka kupitia kununua kazi zake na kufuatilia shughuli zake za kisanaa.
“Nilichojifunza mimi kama msanii ambaye nimefika hapa kwa sapoti ya jamii inayonizunguka kwa kununua kazi zangu na kunifatilia, basi kwenye maisha ninayoishi jamii inathaminiwa zaidi ya kitu chochote.Ni vyema nikaendelea kuwa nayo kwa shida na raha. Nitasimama upande wa haki siku zote,” ameandika Rose.
Kauli hiyo imetafsiriwa kama ishara ya nia ya Rose kuendelea kushirikiana na mashabiki wake na kuichukulia jamii kama nguzo muhimu katika maisha yake ya sanaa na kijamii.
The post Rose Ndauka awashukuru mashabiki first appeared on SpotiLEO.