BARCELONA: WINGA wa mabingwa wa LaLiga FC Barcelona Lamine Yamal hayumo katika orodha ya majina ya kikosi cha timu hiyo kitakachosafiri hadi nchini engaland kwa ajili ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi dhidi ya Newcastle United kesho Alhamisi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 18 alikosa ushindi wa timu yake dhidi ya Valencia Jumapili kutokana na jeraha la misuli ya paja, suala lililomuibua meneja wa Barcelona Hansi Flick aliyekosoa muda ambao Yamal aliichezea timu ya taifa ya Hispania kwenye michezo ya kimataifa.
Yamal aliichezea nchi yake kwa dakika 79 kwenye mchezo walioshinda 3-0 dhidi ya Bulgaria tarehe 4 Septemba kisha dakika 73 za kwenye mechi ya ushindi wa 6-0 dhidi ya Uturuki siku tatu baadaye.
Barcelona ilivuruga Valencia mabao 6-0 bila kinda huyo na haijamjumuisha katika kikosi chao kwa ajili ya mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa msimu huu katika dimba la St James’ Park.
Beki wa kushoto wa Hispania Alejandro Balde na kiungo wa kati Gavi hawapo pia katika orodha hiyo iliyomjumuisha kiungo wa kati wa Uholanzi Frenkie de Jong ambaye alikosa mchezo wa Valencia kufuatia majukumu ya kimataifa.
The post Yamal kuikosa Newcastle kesho first appeared on SpotiLEO.