#TETESI: Kibarua cha kocha Rúben Amorim ndani ya Manchester United kipo hatarini kuota ndago baada ya ripoti Nchini England kueleza kuwa amepewa mechi tatu tu kuokoa kazi yake klabuni hapo huku msururu wa makocha ukitajwa kuwania nafasi hiyo.
Kocha huyo raia wa Ureno ambaye alipewa mikoba hiyo takribani miezi 10 iliyopita ameiongoza Man United kuwa na mwanzo mbaya zaidi wa msimu wa Ligi Kuu England baada ya miaka 33 baada vipigo viwili, sare moja na ushindi mmoja kwenye mechi nne za mwanzo wa msimu.
Inaelezwa kuwa mabosi wa klabu hiyo bado wana imani na kocha huyo wa zamani wa Sporting Lisbon lakini ripoti zinaarifu kuwa uongozi wa klabu hiyo umempa mechi tatu za kujiuliza ili kutathmini mwelekeo wa klabu hiyo kabla ya kufanya maamuzi hatua ambayo pia ilimkuta mtangulizi wake Eric ten Hag.
Wakati huo huo ripoti Nchini England zinaeleza kuwa klabu hiyo imeanza kuwatupia macho machocha watano wakiwemo Oliver Glasner, Marco Silva, Andoni Iraola, Mauricio Pochettino na Gareth Southgate kwa ajili ya kuchukua mikoba ya Mreno huyo.