Benki ya NMB imefanya kongamano maalum na wafanyabiashara wa mkoa wa Tabora, likilenga kujadili fursa za kifedha na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo.
Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara wa NMB, Dickson Richard, akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, amesema benki imejipanga kuendelea kushiri.
kiana kwa karibu na wafanyabiashara katika kuwawezesha kifedha na kukuza biashara zao.
Kongamano hilo limewaleta pamoja wafanyabiashara wa Tabora, likiwa jukwaa la kuimarisha mahusiano na kuonesha nafasi ya benki katika kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa eneo hilo.