DAR ES SALAAM: MSHAMBULIAJI wa KMC aliyeibuka shujaa katika ushindi wa timu yake dhidi ya Dodoma Jiji Darushi Saliboko amesema siri ya bao pekee lililoipa alama tatu katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ilikuwa ni kutumia madhaifu ya wapinzani.
Akizungumza baada ya mchezo huo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa KMC, mfungaji huyo alisema walizingatia maelekezo ya mwalimu wao aliyewataka kutumia nafasi zilizotokana na mapungufu ya wapinzani.
“Tuliangalia madhaifu ya wapinzani wetu, mwalimu akatuambia wanapenda kuacha nafasi. Tulitumia mwanya huo, tukakimbia na kufunga,” alisema mfungaji huyo ambaye pia aliibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kwa matokeo hayo, KMC imeanza msimu mpya kwa kishindo baada ya kuondoka na ushindi muhimu, huku benchi la ufundi likiahidi kuendelea kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza ili kufanya vizuri zaidi katika michezo ijayo ya Ligi Kuu.
Michezo mingine iliyochezwa jana ni Coastal Union iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga. Bao pekee lililowekwa kimiani na Cleophance Mkandala.
The post Saliboko: Tulitumia udhaifu wa Dodoma Jiji first appeared on SpotiLEO.