ZURICH: TIMU ya taifa ya Hispania imeipokonya timu ya taifa ya Argentina nafasi ya kwanza katika viwango vipya vya FIFA kwa timu za wanaume vilivyochapishwa leo Alhamisi, na kuongoza kwa mara ya kwanza tangu mwezi Juni 2014.
Ushindi mara mbili kwa Hispania katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia 2026 mwezi huu dhidi ya Uturuki na Bulgaria umewainua mabingwa hao wa Ulaya kutoka nafasi ya pili nyuma ya mshindi wa Kombe la Dunia 2022 Argentina, ambayo imeanguka hadi ya nafasi ya tatu.
Kipigo cha Argentina katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador pia kumeifanya timu ya taifa Ufaransa kupanda nafasi moja hadi namba 2.
England imesalia namba 4, na Ureno imepanda nafasi moja hadi namba 5 kwa kubadilishana na Brazil, ambayo ilipoteza mchezo dhidi ya Bolivia.
Kutoka Afrika Morocco ndiye kinara, ipo namba 11 ikiwa bora zaidi kwa mataifa ya Afrika na Japan imeongoza kwa mataifa ya Asia ikiwa namba 19. Zote tayari zimefuzu kwa Kombe la Dunia.
Mexico na Marekani wapo namba 14 na 16 huku waandaji hao wenza wa Kombe la Dunia lijalo wakianguka kwa nafasi moja. Canada, mwenyeji mwenza wa tatu wa michuano hiyoya mwaka ujao, Canada imepanda hadi namba26
The post Spain yaipiga ‘gepu’ Argentina viwango vya FIFA first appeared on SpotiLEO.