WIKIENDI imechangamka kwenye anga la kimataifa kutokana na timu zote nne kutoka Tanzania kuwa katika kazi.
Ijumaa, Uwanja wa 11 de Novembro, Wiliete Sports vs Yanga SC, saa 12:00 jioni.
Simba SC Jumamosi Septemba 20 itakuwa uwanjani kumenyana na Gaborone United saa 2:00 usiku.
Yanga SC na Simba SC ni katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni hatua ya awali.
Azam FC wapo Sudan Kusini watacheza dhidi ya Al Merriekh Bentiu Septemba 20 saa 11:00 jioni.
Singida Black Stars wapo Reanda watakuwa na mchezo dhidi ya Rayon Sports Septemba 20 2025.
Azam FC na Singida Black Stars ni katika Kombe la Shirikisho Afrika.
The post WIKIENDI YA MOTO WA CAF HII HAPA….SIMBA, YANGA MGUU SAWA….. appeared first on Soka La Bongo.