MUNICH: KOCHA wa Bayern Munich Vincent Kompany amesema michuano ya kombe la Dunia la Klabu lililofanyika kwa takriban mwezi mzima limekisaidia kikosi chake kupata muunganiko aliohitaji kuanza vyema msimu mpya wa 2025/26.
The Bavarians walikuwa na wachezaji wapya Jonathan Tah na Tom Bischof katika kikosi chao kilichocheza michuano hiyo ya Juni 14 hadi Julai 13 nchini Marekani, ambapo walitolewa katika robo fainali na Paris St Germain.
Timu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Borussia Dortmund, zililalamikia kalenda ya michuano hiyo ambayo kwa mujibu wao ilitoa mfupi wa ‘pre-season’ kuliko kawaida kwa sababu ya ushiriki wao katika Kombe hilo la Dunia la Klabu.
Michuano hiyo iliziacha timu kadhaa bora za Ulaya na wiki nne pekee za kupumzika na kujiandaa na msimu mpya. Ligi nyingi kubwa za Ulaya kawaida huisha mwishoni mwa mwezi Mei.
“Kombe la Dunia la Klabu lilinisaidia katika kuwaingiza wachezaji wapya kikosini. Kuna hisia kwamba wachezaji kama Jonathan Tah na Tom Bischof wamekuwa hapa kwa muda mrefu. Labda inahusiana na ukweli kwamba tulikuwa tunaishi pamoja kwa mwezi mzima nchini Marekani” – Kompany aliuambia mkutano na waandishi wa habari
“Hatuna uhakika namna tutakavyoathirika na Kombe la Dunia la Klabu baadaye msimu huu lakini ninachojua mimi ni tulikaa pamoja kwa mwezi mzima jambo ambalo ni nadra kwa klabu nyingi” – aliongeza.
Chochote kilichopatikana kwenye michuano hiyo huenda kiliwasaidia mabingwa hao kuanza msimu kwa kasi, wakishinda mechi zao zote za Bundesliga na kuwa kileleni mwa ligi hiyo kwa pointi tisa baada ya michezo mitatu na iliifumua Chelsea kwenye UEFA champions league.
The post “Kombe la dunia la Klabu limetusaidia” – Kompany first appeared on SpotiLEO.