LIVERPOOL: MENEJA wa Everton David Moyes amesema kuchukua pointi mbele ya Liverpool siku zote imekuwa kazi ngumu, lakini anafahamu kwamba mabingwa hao watetezi wana udhaifu fulani unaoweza kutumika kuwaadhibu.
Moyes, ambaye ameshinda mechi sita pekee kati ya 44 alizokabiliana na Liverpool katika maisha yake ya ukocha, amesema safari yake hiyo ya Anfield itasaidia kupima ubora wa Everton baada ya timu yake kuvuna pointi saba katika mechi nne za kwanza za ligi.
“Kama ambavyo Liverpool wameonesha ukali wao kwa nyakati tofauti, wakati mwingine wameonesha udhaifu fulani wameruhusu mabao pia” Moyes aliwaambia waandishi wa habari.
“Sisi pia tujaribu kutumia udhaifu huo. Tulicheza nao mwaka jana Anfield na tukapoteza kwa bao la kuotea, tunataka kuwafunga tena pengine safari hii mambo yatakuwa upande wetu.”
Liverpool, ambao wameshinda michezo yao yote minne ya ligi hadi sasa, walipata ushindi dhidi ya Everton katika mchezo wa mwisho uliozikutanisha timu hizo walipoilaza timu hiyo ya David Moyes kwa bao 1-0 kutoka kwa Diogo Jota kipindi cha pili mwezi Aprili mwaka huu.
The post “Liverpool wana udhaifu” – Moyes first appeared on SpotiLEO.