TANGA: MABONDIA 27 wametinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya klabu bingwa taifa inayoendelea kupigwa kwenye Uwanja wa Urithi mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania BFT Lukelo Willilo, katika mabondia waliotinga hatua ya nusu fainali sita wanatoka klabu za MMJKT na Ngome, Magereza ikiwa na mabondia watano.
JKT Mgulani (Dar es Salaam m) na Jeba Boxing (Tanga) wanafuatia kwa kuwa na mabondia wawili kwa kila timu huku Band Coy (Dar es Salaam), Ngamiani (Tanga) na Chang’ombe Boxing wakiwa na bondia mmoja kutoka kila timu.
Mashindano haya yanatarajiwa kufikia hatua ya fainali na kumpata bingwa wa Taifa wa 2025 siku ya Jumamosi kesho.
Lekelo amesema ushindani umekuwa mkubwa kwa mabondia wakionesha vipaji vya hali ya juu.
Amesema anategemea fainali kali hiyo kesho yenye ushindani kutoka katika klabu hizo zenye mabondia wengi kama ambavyo zimeonesha katika michezo iliyopita.
Awali, kulikuwa na mabondia 97 walioshiriki hatua za awali.
The post Mabondia 27 watinga hatua ya nusu fainali klabu bingwa Taifa first appeared on SpotiLEO.