DAR ES SALAAM : MSANII wa video na mrembo maarufu, Nicole Joyberry, ameandika ujumbe wa upendo na shukrani kwa rafiki yake wa karibu, Jacqueline Wolper, akimsifu kwa hekima, utu na upendo alioonyesha katika urafiki wao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nicole amesema alitumia muda kumchunguza Wolper kabla ya kumkaribisha kama rafiki wa dhati. “Nilituliza sana kichwa wakati namchagua huyu best friend wangu Wolperstylish. Nilimtathmini kama vile nachagua mchumba,” ameandika Nicole, akifafanua kuwa alizingatia maneno, vitendo na namna Wolper anavyowatendea watu.
Amesema Wolper ni mtu mwenye busara na moyo wa upendo, akibainisha hata katika mambo madogo kama kupiga picha pamoja, huonyesha msaada na kujali. “Huwa namchokoza tu mara nyingine, nimuulize kuhusu watu fulani… jibu lake huwa na hekima, halina chuki. Ana upendo mia fil mia,” ameongeza Nicole.
Kwa mujibu wa Nicole, urafiki wao umejengwa kwenye misingi ya imani na maombi, akifichua kuwa Wolper amekuwa akiomba kwa ajili yake hata usiku wa manane. “Jana saa nane usiku amenipigia simu, akaniambia: ‘BFF soma Zaburi 35 halafu lala.’ Nilikuwa safarini, ndege ikatua saa 10 usiku, hakulala mpaka nimemwambia nimefika salama,” amesema.
Nicole ameendelea kumsifu Wolper kama mwamba, mwalimu, mama bora na rafiki wa kweli, akiwataka watu kutulia na kuwa makini wanapochagua marafiki. Katika hitimisho lake, ameandika methali ya siku: “Maombi tunayoyaomba, sisi ni wa juu milele!”
The post Nicole afunguka urafiki na Wolper first appeared on SpotiLEO.