Wagombea hao, ambao walitua kwa Chopa na kuzua taharuki ya shangwe wametajwa kuwa tegemeo kubwa sana katika jimbo hilo.
Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Ndugu Michael Lushinge (Smart), ambaye alisisitiza mshikamanano, mshikamano na ari ya ushindi wa chama katika uchaguzi ujao.
Mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi na wagombea mbalimbali wakiwemo:
- Madiwani wa kata zote 30 za Wilaya ya Kwimba (ambayo ina majimbo mawili: Kwimba na Sumve).
- Moses Bujaga, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Sumve.
- Wagombea Udiwani viti maalum.
- Wagombea Ubunge viti maalum Mkoa wa Mwanza.
- CDE Seth B. Masalu, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mwanza.
- Mhe. Kasalali Mageni, Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumve.
- Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mwanza.
Wananchi walionyesha imani kubwa kwa wagombea wao na kuahidi kushiriki kikamilifu katika kampeni na uchaguzi, kuhakikisha ushindi wa kishindo kwa wagombea wote wa CCM katika jimbo hilo.

Kwa unyenyekevu mkubwa kijana Cosmas Bulala, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba, akiomba kura kwa wananchi
Kwa unyenyekevu mkubwa kijana Cosmas Bulala, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kwimba, akimwaga sera na kuomba kura kwa wananchi
