Kocha wa Manchester United Ruben Amorim anasema ana matumaini ya kupata muda wa kuonyesha jinsi mfumo wake utakavyobadilika, lakini anasisitiza hata Papa hataweza kumfanya abadilishe mfumo wake.
Mojawapo ya shutuma za kocha huyo Mreno ni kwamba ameng’ang’ana mno na mfumo wake wa 3-4-3 na anapaswa kubadilika.
Hata hivyo kocha huyo mwenye umri wa miaka 40 alikiri kuwa ana wasiwasi na kile wachezaji watafikiria ikiwa ataamua kubadili mfumo.