KUONDOKA KWA FADLU: “….hakuna mahali popote ambapo klabu yetu itaathirika…..tunakwenda kutafuta kocha bora zaidi ambaye ataifikisha Simba kwenye nchi ya ahadi”
Simba SC yatoa ufafanuzi kuhusu kuondoka kwa kocha wake Fadlu Davids ikisema haikuwa imejiandaa kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi.
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally amezungumza ‘LIVE’ na #Mshikemshike ya #AzamSports1HD na kusema tayari mipango ya kutafuta mbadala wa kocha huyo, imeanza na “Hadi kufikia tar 28, tutakuwa tumepata kocha mpya…”
Ahmed amewatoa hofu mashabiki akiwataka kuwa watulivu kwakuwa kilichotokea ni kitu cha kawaida na klabu haijatetereka kwa kuwa imejengwa kitaasisi…
Amesema kwa sasa timu itabaki chini ya Selemani Matola ambaye ndiye ataiongoza katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate….
Kuhusu wachezaji waliosajiliwa kwa mapendekezo ya kocha Fadlu, Ahmed ameuweka wazi ujumbe ambao uongozi wa klabu hiyo tayari umewaeleza wachezaji hao.