DAR ES SALAAM, MREMBO na mwanamitindo maarufu nchini, Sanchoka, ameweka wazi hisia zake kwa kudai kuwa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba, ndiye msanii wa kiume anayemvutia zaidi kimapenzi.
Kauli hiyo imezua gumzo mitandaoni, baada ya Sanchoka kueleza wazi kuwa mvuto wa Alikiba unamfanya kumtamani zaidi ya wanaume wengine maarufu nchini.
Akizungumza kupitia mahojiano, Sanchoka amesema mvuto wa Alikiba unatokana na muonekano wake wa kuvutia pamoja na tabia ya kutojihusisha na drama nyingi za mitandaoni.
“Hakuna mwanaume maarufu mwenye mvuto kumzidi Alikiba. Jamaa ana muonekano mzuri mno na hana mambo mengi kabisa. Hayo ndiyo hunifanya nizidi kumtamani kimapenzi,” amesema Sanchoka.
Kauli hiyo imeendelea kuchochea mijadala miongoni mwa mashabiki, baadhi wakikubaliana naye huku wengine wakionesha mitazamo tofauti.
The post Sanchoka: Alikiba ndiye msanii mwenye mvuto zaidi first appeared on SpotiLEO.