Klabu ya Simba Sc imethibitisha umefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Mkuu Fadlu Davids kama kocha mkuu klabuni hapo na kubainisha kwamba makubaliano hayo ni matakwa binafsi ya kocha Fadlu kwa uongozi wa klabu hiyo
Simba Sc imethibitisha hilo kupitia taarifa yake kwa umma ya leo Septemba 22, 2025 huku ikimshukuru kocha huyo kwa kuiongoza klabu hiyo kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na kumalizia nafasi ya pili kwenye Ligi kuu ya NBC.
Aidha uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi umemtakia kheri na baraka kocha Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini katika maisha yake ya soka nje Simba