WACHEZAJI wawili raia wa Afrika Kusini, Neo Maema na Rushine De Reuck, amewaahidi wanachama na mashabiki wa Simba kuwa watarajie ushindi mwingine katika mchezo wa marudiano dhidi ya Gaborone United ya Botswana, Jumapili ijayo, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa kwanza, hatua ya awali, Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone, uliopigwa juzi na kupata ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Obed Itani Chilume, mjini Francistown, wachezaji hao waliosajiliwa msimu huu wakitokea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, walisema haikuwa rahisi, kwani walicheza na timu ngumu.
Walisema wanaifahamu timu hiyo na baadhi ya wachezaji wanafahamiana nao, ambapo haina tabia ya kupoteza ikicheza uwanja wake wa nyumbani, lakini wao wamevunja mwiko huo, huku wakiahidi kufanya hivyo wakicheza jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya marudiano.
“Tumefanya kila tunachoweza, tumecheza vizuri, haikuwa mechi rahisi kwa sababu wapinzani wetu walikuwa bora pia. Ni timu yenye wachezaji wenye uwezo mkubwa, ni ngumu kufungika inapocheza nyumbani kwao,” alisema Rushine, beki wa kati wa timu hiyo ambaye ameanza kuwa kipenzi cha wanachama na mashabiki wa Simba kutokana na uwezo mkubwa alioonesha juzi na michezo iliyopita ya Simba Day dhidi ya Gor Mahia na Yanga, kwenye mechi ya Ngao ya Jamii.
Kiungo mshambuliaji, Maema, alisema mechi hiyo ilikuwa kipimo kizuri kwao na matokeo ya ushindi yamewapa matumaini ya kwenda raundi ya kwanza, kwani yamewarahisishia kazi kuelekea mchezo wa marudiano.
“Kilikuwa ni kipimo kizuri kwetu kama timu, tumepata matokeo ya ushindi, imetupa matumaini na kuturahisishia kazi kuelekea mchezo wetu wa marudiano. Najua bado tuna safari ndefu, lakini hiki tulichokipata ni bora zaidi,” alisema mchezaji huyo.
Aliongeza kuwa mechi haikuwa rahisi, hasa kipindi cha pili kwani wapinzani wao waliamua kufunguka na kushambulia baada ya kuona hawana cha kupoteza.
“Wapinzani wetu walikuwa bora zaidi kipindi cha pili, kwa sababu tayari walikuwa wameshafungwa bao na waliamua kushambulia kwa sababu walikuwa nyumbani, na walijua wakipoteza watapata wakati mgumu kwenye mchezo wa marudiano, nafikiri mabeki wetu walifanya kazi nzuri sana. Hawa jamaa ni hatari wakiwa kwao, tunawajua na hata wachezaji wao tunafahamiana nao sana,” alisema Maema.
Bao pekee la Simba kwenye mchezo huo liliwekwa wavuni na winga wa Kikongomani, Elie Mpanzu akiunganisha krosi ya Shomari Kapombe.
Wakati huo huo, Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo amewataka wanachama na mashabiki wa Simba kuwa watulivu wakati wakisubiri majibu kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu (CAF), kama mechi ya marudiano itakuwa na mashabiki au la.
CAF ilitangaza kuwa mechi hiyo haitokuwa na mashabiki kutokana na adhabu ambayo wameipa klabu hiyo baada ya mashabiki wake kudaiwa kufanya fujo, lakini Ahmed alisema suala hilo wamelikatia rufaa.
“Ni kweli tulipokea taarifa kutoka CAF kuwa mechi yetu ya marudiano hatutoruhusiwa kuingiza mashabiki, kwa sababu ya adhabu ambayo tumepewa, lakini tulianza mazungumzo nao, ikiwamo kukata rufaa, hivyo tunasubiri majibu ili tuwe kwenye nafasi nzuri ya kuwatangazia mashabiki kama mechi inaruhusiwa mashabiki au la,” alisema.

The post BAADA YA KUANZA KINYONGE CAF….WASAUZI WA SIMBA WAFUNGUKA YA MOYONI…. appeared first on Soka La Bongo.