Bado nawashangaa wanaosema Roman Folz ameishindwa Kuicontrol Yanga , ndio kwanza ana game mbili za kimashindano na zote amepata ushindi na Cleansheet huku akifunga magoli manne 👏 Kafanikiwa : Nafikiri ni ngumu kocha kujiunga na timu then hapo hapo uanze kuona vitu chanya .
Wakati Klopp anajiunga na Liverpool alihitaji muda ili kuwapa mafanikio vijana wa Anfield nyakati ambazo walikuwa na ukame wa kwenda misimu zaidi ya 10 bila kombe la ligi .
Msimu wa kwanza wa Pep na City ulikuwaje ? Si bado alistruggle eee 😀 vipi Enrique na PSG yake iliyokuwa tishio msimu uliopita ? Kwahiyo sio rahisi kocha kuja na timu kuclick hapo hapo . Inatokea mara chache sana ( Bonus )
Kinacho matter ni matokeo ya Ushindi kwanza na kuendelea kutengeneza falsafa yake kwenye timu …. Roman bado hajapata first Eleven yake ndio maana unaona kikosi kinajirudia kile kile cha msimu uliopita .
Football ni mchezo katili sana unaweza kujaribu bila kuwa na taadhari then ikakupalia 🙌 nilichoona kipya kwa Roman japo sio kwa ukubwa sana ni:
1: Kuna muundo mzuri wa kuzuia ( Pale wanapopoteza mpira “Counter Pressing , Idadi nzuri ya wachezaji wakati wanafanya Pressing then anahitaji timu inayoshambulia kwa kasi sana )
2: Wakiwa na mpira uharaka wa maamuzi na runners wanakuwa wengi eneo la juu : Positioning ya FBs na wale mawinga wao inatoa msingi mzuri wa kutengeneza “Overload” pembeni ya kiwanja .
3: Idadi ya wachezaji eneo la mbele na ndio maana wamekuwa na Accurate nzuri ya kutengeneza nafasi but Ufanisi umekuwa mdogo kwa wachezaji wa mbele .
HAKUNA TIMU INATENGENEZWA KWA KIPINDI KIFUPI .