Nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto, amesema wanataka kuanza kwa kishindo mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu tanzania dhidi ya Pamba Jiji kama walivyofanya kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuichakaza Wiliete de Benguela ya Angola mabao 3-0.
Akizungumza kuelekea mchezo huo utakaopigwa kesho Jumatano, Mwamnyeto anasema kama wameanza kwa kishindo kwenye ligi ya Mabingwa kwa kumpiga mtu mabao 3-0, basi wanataka kuendeleza kishindo kwenye Ligi Kuu dhidi ya Pamba, mchezo unaotarajiwa kupigwa, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
“Tumeambizana wachezaji wenyewe hakuna kulala, mechi msimu huu zitakuwa nyingi na hakutakuwa na muda mrefu wa kupumzika, nadhani inaweza kuwa kila baada ya siku tatu, mambo ni mengi lakini muda ni mchache,” alisema Mwamnyeto.
Alingeza; “Kwa maana hiyo tumetoka kucheza mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika tumeshinda mabao 3-0, sasa tunakwenda kucheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya Pamba, tunataka kilichotokea kule Angola ndicho kitokee huku.”
NIPASHE