DAR ES SALAAM: Msanii wa kizazi kipya mwenye makazi yake Atlanta, Marekani, Dogo Red, ametamba kutikisa Afrika Mashariki kupitia video ya wimbo Vanessa aliowashirikisha nyota kutoka Burundi, Wiz Designer na Rich Forever.
Dogo Red, ambaye ni miongoni mwa wasanii wachache wa Afrika Mashariki wanaofanya muziki ughaibuni kwa mafanikio, amesema video hiyo itazinduliwa rasmi Ijumaa hii.
Akizungumza na Spoti Leo, msanii huyo ambaye pia ni bosi wa lebo ya Wapamba Classic, amesema audio ya Vanessa ilipokelewa kwa kishindo na mashabiki katika majukwaa mbalimbali ya kusikiliza muziki duniani, na sasa wanataka kuona video yake.
“Nimejibu kiu ya mashabiki kwa kuachia video hii. Nitaiachia Ijumaa hii kupitia chaneli yangu ya YouTube, hivyo mashabiki wangu pamoja na wale wa Wiz Designer na Rich Forever watakata kiu yao ya muda mrefu,” amesema Dogo Red
The post Dogo Red na ndoto za kuitawala Afrika Mashariki first appeared on SpotiLEO.