DAR ES SALAAM: KOCHA Msaidizi wa Simba Seleman Matola amesema kikosi chake kiko tayari kupigania pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Fountain Gate utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam leo Matola amesema: “Maandalizi yetu yamekwenda vizuri na tupo tayari kuhakikisha tunapata alama tatu,”
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji David Kameta amesema kila mchezaji anatambua kuwa hautakuwa mchezo rahisi lakini wapo tayari kupata pointi tatu.
Simba inakwenda kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu chini Kocha mpya wa muda Mohamed Morocco aliyeteuliwa baada ya aliyekuwepo Fadlu Davis kutimkia Raja Cansablanca.
Kabla ya kuondoka, aliongoza Simba kushinda mchezo wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United walioshinda bao 1-0.
Wekundu hao wa Msimbazi walisema jana kuwa Kocha Matola hatakuwepo katika mchezo huo wa ligi kwasababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu.
The post Matola: Tuko tayari kupigania pointi tatu first appeared on SpotiLEO.