Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kimetangaza kuwa Hafla ya Tuzo za Shirikisho hilo (TFF Awards 2025) itafanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba ambapo Tarehe ya hafla hiyo ya kutambua wanamichezo waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali kwa msimu wa 2024/2025 itatangazwa baada ya kukamilisha maandalizi mengine ikiwemo ukumbi.
Taarifa ya leo Septemba 23, 2025 iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa katika hafla hiyo, zitatolewa tuzo katika makundi nane ya Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB, Ligi Kuu ya Wanawake, Ligi ya NBC ya Championship, First League, Ligi ya U20 ya NBC, na tuzo za Utawala.
Mchezaji Bora (MVP) kwa msimu wa 2024/2025 atafahamika usiku wa tuzo hizo ambazo huwakutanisha wadau mbalimbali wa mpira wa miguu ikiwemo Serikali pamoja na wadhamini.