Simba Wanamtaka Kocha Aliyeipeleka Fainali MADAGASCAR Kombe la CHAN
Licha ya makocha wengi kuomba nafasi ya kuifundisha Simba, uongozi wa klabu hiyo upo kwenye mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya MADAGASCAR ๐ฒ๐ฌ ROMUALD RAKOTONDRABE, aliyeiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya pili kwenye michuano ya CHAN 2024 iliyofanyika mwaka huu katika nchi za TANZANIA ๐น๐ฟ, KENYA ๐ฐ๐ช na UGANDA๐บ๐ฌ.
Chanzo changu cha ndani kimesema โSimba inatafuta kocha haraka ambaye atakuja kabla ya mchezo wa marudiano na kuna uwezekano tukamalizana na kocha wa MADAGASCAR ๐ฒ๐ฌ.
โMOROCCO amekuja kwa ajili ya mechi moja pekee ya marudiano dhidi ya GABORONE UNITED, baada ya hapo timu ndiyo itaendelea kufundishwa na huyo kocha mpya ndiyo maana mchakato unafanyika kwa haraka sana.
โWakati mchakato ukiendelea na ujio wa MOROCCO, kwa asilimia kubwa MATOLA atakuwa akitoa msaada wa kuijenga timu kwani amekuwa nayo kwa muda mrefu, hivyo hata kama hatokuwa kwenye benchi Jumapili, lakini katika uwanja wa mazoezi atasaidia pakubwa sana.โ
Endapo SIMBA SPORTS CLUB itamalizana na Kocha RAKOTONDRABE, basi kibarua chake cha kwanza kinatarajiwa kuwa Oktoba Mosi 2025 dhidi ya Namungo, katika mchezo wa Ligi Kuu utakaofanyika uwanja wa BENJAMIN MKAPAย
Julai Mosi 2025, RAKOTONDRABE mwenye umri wa miaka 60, aliteuliwa kukiongoza kikosi cha MADAGASCAR ๐ฒ๐ฌ kushiriki michuano ya CHAN 2024 na kukifikisha fainali, kikapoteza mbele ya MOROCCO. Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA Pro, amekuwa akipenda kutumia mfumo wa 4-3-3โฆ
โย






