Mwakilisha wa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Dominick Njunwa akizungumza katika mahafali jijini Arusha.
Mkurugenzi wa shule ya Msingi na Sekondari katika shule ya Trust St. Patrick Mike Patrick akizungumza kwenye mahafali.
Mkuu upande wa shule ya awali,Lucy Kessy akizungumza na wazazi pamoja na wanafunzi katika mahafali hayo jijini Arusha.
………..
Happy Lazaro, Arusha
WANAFUNZI wanaohitimu masomo yao nchini wametakiwa kujiepusha na makundi yasiyofaa ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya,ulevi ,pamoja na ndoa za jinsia moja kwani vitawaharibia malengo yao ya baadaye.
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Dominick Njunwa ambaye alimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mwinyi Ahmad Mwinyi kwenye mahafali ya wanafunzi wa awali, msingi na sekondari katika shule ya Trust St.Patrick iliyopo jijini Arusha.
Amesema kuwa, wanafunzi wengi wanapohitimu wamekuwa wakijiachia kwa kuona kuwa ndio mwisho wa masomo yao kitendo ambacho amesema kuwa hapo ndio mwanzo tu hivyo wanapaswa kupambana zaidi na kujiendeleza kwani ndio kwanza safari yao imeanza.
Dominick amewataka pia kuepuka wimbi la mapenzi ya jinsia moja ambalo limeshika kasi sasa hivi ni muhimu kuyazingatia hayo kwa manufaa yao na wajue kuwa kila kitu kina wakati wake.
Aidha akizungumza kuhusu barabara ya shule hiyo ambayo imekuwa ni changamoto kwa magari ya shule kutokana na miundombinu mibovu amesema kuwa swala hilo atalifikisha katika ofisi ya mkuu wa wilaya ili iweze kufanyiwa kazi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule hiyo, Mike Patrick amewataka wahitimu wote kuhakikisha wanakuwa na nidhamu.na uwajibikaji kwani ndio silaha ya mafanikio na kuhakikisha wanayaendeleza yale yote waliyoyapata hapo shuleni na kuwa mabalozi wazuri wa kutangaza shule hiyo.
Mike amesema kuwa ,shule ya Trust St. Patrick ina wanafunzi wa darasa la awali,msingi pamoja na sekondari na imekuwa ikifanya vizuri kwa kuwaandaa wanafunzi wake kwa vitendo iliwaweze kujitemea pindi watakapomaliza masomo yao na kuepuka kuwa tegemezi kwenye familia zao.
“Shule hii imekuwa ikifundisha wanafunzi nadharia na vitendo na kwa kufanya hivyo maswala mbalimbali ikiwemo ushonaji,utengenezaji keki, ambapo inawawezesha kuweza kujitemea kwa maisha yao ya baadaye .”amesema.
Kwa upande wake Mtawala wa shule hiyo ,Dokta Dinnah Mosha amesema kuwa ,shule hiyo imefikisha miaka 28 tangu kuanzishwa kwake.
Amesema kuwa shule hiyo inasimamia vizuri sana nidhamu ya watoto na kuanzia elimu ya awali hadi darasa la saba wamekuwa wakijifunza elimu ya kujitegemea.
Amesema kuwa hawawaandai kwa nadharia peke yake bali.wanawafundisha kwa vitendo ili kuwasaidia kuweza kutafuta soko la ajira badala ya kutegemea kuajiriwa pale wanapomaliza elimu yao.
Ameongeza kuwa, wamekuwa wakifundisha maadili ili wasijekuwa mzigo katika familia zao ambapo kutokana na changamoto za kidunia wamejipanga sana kuwandaa watoto hao na kuwavusha katika kizazi hiki.chenye changamoto kubwa sana.
Aidha amewataka wazazi pamoja na walezi kufuatilia kwa karibu mienendo ya watoto wao kwani swala la malezi ni la wazazi kutoka pande zote mbili huku akiwataka wazazi kujitahidi migogoro yao isiwe kikwazo kwa watoto kwani inawafanya wanashindwa kufanya vizuri katika masomo.
“Naombeni sana swala la ugomvi unaotokea kati ya wazazi zinawapelekea watoto hawa kupita katika wakato mgumu sana hivyo basi tunaomba wazazi wenzangu pamoja na cha changamoto zote tujitahidi sana kuzuia migogoro yetu isiwaathiri watoto kwani kuna baadhi ya watoto wanafikia hadi hatua ya kutaka kujiua na wamekata tamaa kutokana na migogoro ya familia.”amesema.
Amefafanua kuwa shule hiyo imekuwa ikiwaandaa watoto kuweza kujitegeme ili ikitokea hata siku ambayo wazazi hawapo watoto wasiteseke.
“Shule hiyo imeingia ushirikiano na shule rafiki ya China ambapo kila mwezi Juni wanaenda kutembelea nchi hiyo na kwenda kujifunza maswala mbalimbali ikiwemo ujasiriamali na kupata uzoefu ambapo mwaka jana walipeleka wanafunzi 40 na walimu 4 ambapo waliweza kujifunza mambo mbalimbali na waliweza kuona jinsi watoto wadogo walivyoweza kujitegemea na kuweza kufanya mambo makubwa sana”amesema Dokta Dinnah.
Naye, Mkuu upande wa shule ya awali,Lucy Kessy akizungumza katika mahafali hayo amesema kuwa, amesema kuwa kitaaluma.wanafanya vizuri ambapo wanajua mtoto sio taaluma lakini pia hata michezo hivyo shule inajihusisha na mambo ya michezo ambapo wanafunzi wanafanya michezo mbalimbali kwa ajili ya kuchangamsha akili zao.
Kwa upande wa taaluma wanahakikisha kila mtoto wao anafanya kwa kiwango cha juu kuhakikisha kwamba elimu wanayopata haiiwi elimu tu ya darasani ila inakuwa mpaka elimu ya kimaisha na anajua namna ya kujitegemea na kupambana na ulimwengu.
Aidha amewaasa wanafunzi kuwa hiyo ni hatua moja ndo wamemaliza popote wanapofika waendelee kuonyesha zile juhudi walizokuwa wakionyesha hapo shuleni waziendeleze huko kote watakapokuwa waendelee kutia juhudi pamoja na nidhamu waliyofundishwa.