LONDON: KLABU bingwa ya Dunia Chelsea imeamua kumpumzisha kiungo mashambuliaji wake Cole Palmer kwa wiki mbili hadi tatu zijazo ili kumsaidia kupona kabisa jeraha alilopata mwezi uliopita.
Kiungo huyo wa kimataifa wa England, alipata jeraha la misuli ya kitovu (groin) mwezi uliopita, lakini alirejea uwanjani na kufunga mabao mfululizo dhidi ya Brentford na Bayern Munich. Hata hivyo, mchezaji huyo mwenye miaka 23 alilazimika kuondoka uwanjani akiwa na jeraha walipopoteza 2-1 dhidi ya Manchester United Jumamosi.
“Ndiyo, tumeamua kumlinda kidogo Cole. kuhakikisha jeraha lake halizidi kuwa baya. Tumeamua kumpumzisha kwa wiki mbili hadi tatu mpaka mapumziko ya kimataifa tuone kama kwa mapumziko hayo yanaweza kumsaidia kupona kikamilifu na kuwa na afya” – Maresca aliwaaambia waandishi wa habari kabla ya mechi ya nyumbani ya dhidi ya Brighton.
“Sidhani kama anahitaji upasuaji, lakini ni kwa ajili ya kudhibiti maumivu ya kitovu tu. Tumeamua kuwa nae makini kidogo.” – aliongeza
Beki Tosin Adarabioyo pia huenda atakuwa nje mpaka mapumziko ya kimataifa, yanayonza Oktoba 6, kutokana na tatizo la misuli ya kifundo cha mguu, huku Wesley Fofana akipata concussion wakati wa ushindi wa 2-1 wa Kombe Carabao dhidi ya Lincoln City Jumanne.
Washindi hao wa Kombe la Dunia la Klabu ambao wamekusanya pointi nane katika mechi zao tano za mwanzo za Ligi Kuu ya England, pia hawatakuwa na Levi Colwill, Liam Delap na Dario Essugo kutokana na majeraha.
The post Chelsea yampa likizo Palmer first appeared on SpotiLEO.