LIVERPOOL: KOCHA Arne Slot wa Liverpool amesema beki Giovanni Leoni wa klabu hiyo huenda akawa nje ya uwanja kwa takriban mwaka mzima baada ya kupata jeraha la ACL kwenye mguu wake wa kushoto.
Beki huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 18, aliyejiunga na Liverpool msimu huu kutoka Parma, alicheza mechi yake ya kwanza katika ushindi wa Kombe la Carabao dhidi ya Southampton Jumanne, lakini alilazimika kutolewa dakika ya 81 baada ya kuanguka vibaya akiwania mpira.
“Hayupo katika hali nzuri, kwa sababu amevunjika ACL, jambo linalomaanisha atakosa kucheza kwa takriban mwaka mzima,”
“Ukizingatia kuwa bado ni mdogo, amekuja katika nchi mpya, na kucheza vizuri sana katika mechi yake ya kwanza. Ni ngumu kuuona upande mzuri wa jambo hili, kwa kweli haupo lakini kila mara zote ni lazima ujaribu kuelewa. Upande mzuri ni kuwa bado ana umri mdogo na bado kuna miaka mingi mbele yake baada ya kupona jeraha hili baya.” – Slot amesema.
Kwa mujibu wa kocha huyo, muda wa kupona kwa Leoni unamaanisha Liverpool inasalia na mabeki wa kati watatu tu wa uhakika hadi dirisha dogo la usajili la Januari nao ni Virgil van Dijk, Ibrahima Konaté na Joe Gomez.
Slot pia amesema Liverpool inafikiria kumuingiza winger Federico Chiesa kuchukua nafasi ya Leoni kwenye kikosi cha timu hiyo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu.
The post Leonni amtia kiwewe Slot first appeared on SpotiLEO.