Anaandika @kelvinrabson_
✍️ Nafikiri Yanga SC wanatakiwa kuboresha zaidi hasa pale wasipokuwa na mpira , kuna nafasi kubwa kwenye maeneo yote matatu ilikuwa rahisi kwa Wiliete kuifikia defense ya yao kirahisi …. Kivipi ?
1: Wanakuwa wapo mbali mbali baina ya mchezaji mmoja na mwingi , hapo wakipoteza umiliki wa mpira ngumu kuurejesha .
2: Hata maamuzi yao yanakuwa sio sahihi ( Pass na movement )
3: Kunakuwa na ugumu wa kutengeneza connections kuanzia eneo la chini : Kuunganisha pasi zao kutokea eneo la chini .
✍️ Wakiwa na mpira wachezaji wa mbele wanaingia ndani kwenye “Half Spaces” wakiwa kwenye mstari mmoja na namba 10 ( Pacome , Maxi na Abuya ) wakati huo Fullbacks wanakuwa kama wingers .
✍️ Baada ya hapo Yanga wanakosa usahihi wa maamuzi yao ya mwisho : FBs wao cross zao hazikuwa nzuri , maamuzi yao ndani ya box hayakuwa sahihi then Ufanisi ulikuwa mdogo mbele ya goli .
✍️ Wiliete walianza vizuri mchezo sana , bila mpira wanakuwa na muundo mzuri wa kuzuia , utulivu wakati wanaanza build up na waliongeza usahihi wa pasi zao kusogea eneo la juu kirahisi : tatizo ni wakifika kwenye eneo la mbele ( walipoteza mipira kirahisi , walikosa Quality ya kuifungua defense ya Yanga walihitaji mchezaji mwenye uwezo wa kucheza kwenye maeneo finyu na kufanya vitu vitokee )
NOTE :
1: Aziz Andambwile anazidi kuimprove performance yake 👏 utulivu akiwa na mpira , usahihi wa pasi zake na nidhamu nzuri ya kuzuia nafasi .
2: Edmund John kacheza game nzuri sana ✅
3: Chikola zile cross zake 🙌 Kasi + nguvu kwenye mpira ( kacheza game nzuri )
4: Pacome anafanya vitu vitokee kwa urahisi 👏
5: Waliete walikosa QUALITY tu!.. walikuwa na game bora hasa kipindi cha kwanza .
6: BOKA anatakiwa kuboresha pasi zake za mwisho .
FT: Yanga SC 2-0 Wiliete ( Agg 5-0 )
Uchambuzi By : @kelvinrabson_