FIFA inataka kufanya mabadiliko makubwa ya sheria kwa mikwaju ya penalti: kupiga marufuku magoli yaliyofungwa kutokana na rebounds. Ikiwa penalti kipa ataokoa ndio inakuwa shughuli imeisha kwa mpigaji aliyekosa kwa mchezo utaanza tena kwa kibali cha golikipa.
Marekebisho haya, yanayoungwa mkono vna mkuu wa waamuzi Pierluigi Collina, yanalenga kurahisisha maamuzi ya waamuzi na kuwapendelea walinda mlango.
Hata hivyo, kuhusu mpira ambao unagonga mwamba bila kipa kuokoa bado muafaka wake hutajapatikana kiwa itaidhinishwa, mabadiliko hayo yanaweza kuanza kutekelezwa katika msimu wa 2026/27, na kufanya Kombe la Dunia la 2026 kuwa la mwisho kutumia sheria za sasa za adhabu.