Gaborone walianza game vizuri sana na waliingia tofauti na mchezo wa kwanza “Suprise” ni vile walikosa usahihi wa maamuzi yao kwenye actions zao za mwisho …. Kivipi ?
1: Walipata urahisi wa kuivuka pressing wakiwa na watu watatu nyuma dhidi ya wawili wa Simba 3 vs 2 hapo wanapata rahisi kwao kufika eneo la mwisho .
2: Kwasababu Simba wanakuwa na space kubwa kati ya viungo na washambuliaji wao , Gaborone hawakuitaji ufanisi mkubwa wa pasi zao kuivuka pressing ya Simba na walipata space kwenye mpira wakati wa build up yao .
3: Wingers wa Simba ( Morice & Mpanzu) wanachelewa kutrack back kuwasaidia Fullbacks wao hapo inakuwa rahisi kwa Gaborone kutengeneza muunganiko mzuri pembeni ya kiwanja ( Combination Play ) rahisi kwa Gaborone kutengeneza mashambulizi yao kupitia pembeni .
4: Simba walikuwa wanapoteza pasi kirahisi hasa wakati wanaunda mashambulizi kuanzia eneo la chini ( Hakuna Connection ya pass zao kuanzia chini then wanakuwa na idadi ndogo ya wachezaji eneo la juu ) .
✍️ Nafikiri Gaborone walistahili kuimaliza game kipindi cha kwanza : walipata space kubwa wakati wanashambulia , wanafika kwenye eneo la mwisho kirahisi pia walikuwa na idadi nzuri ya wachezaji kwenye kiungo dhumuni ni kutengeneza combination play kwenye maeneo yote ( Pambeni na kwenye kiungo )
✍️ Gaborone United walikosa utulivu na maamuzi sahihi wakifika kwenye eneo la mwisho lakini kirahisi tu , wangekuwa na matumizi mazuri ya nafasi game ingemalizika kipindi cha kwanza .
NOTE :
1: Moussa Camara kafanya baadhi ya saves nzuri kuwaweka
Simba mchezoni
2: Ni kama Fitness level ya wachezaji wa Simba ipo chini sana ( ngumu kuwaona wakishinda mipambano yao kiwanjani ) .
3: Morice Abraham anacheza na haiba, anasimama na kuhesabiwa kama mmoja wa wachezaji viongozi
4: Kikubwa wamefuzu hatua inayofata, wanatakiwa kuboresha performance yao .
5: Umaliziaji wa kiwango cha chini kwa baadhi ya nafasi ulifanya mechi kuwa ya presha kwa Simba
FT: Simba 1-1 Gaborone Utd ( Agg 2-1)
By Kelvin Rabson