HARARE:TANZANIA imehitimisha hatua ya makundi kwa kupoteza mchezo wake wa mwisho dhidi ya wenyeji Zimbabwe kwa tofauti ya mikimbio 113, katika mashindano ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia la wanaume ( ICC Men’s T20 Africa Qualifier) yanayoendelea jijini Harare, Zimbabwe.
Pamoja na matokeo hayo, vijana wa Tanzania wameacha alama ya ushupavu baada ya kupata ushindi wa kuvutia dhidi ya Botswana na Uganda katika michezo ya awali ya kundi.
Ushindi huo miwili uliiwezesha timu kusonga mbele na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa.
Wadau wa mchezo huo wamesisitiza kuwa hatua iliyofikiwa ni kielelezo cha maendeleo ya mchezo wa kriketi nchini, huku mashabiki wakihimizwa kuendelea kuiunga mkono timu hiyo katika safari ya kuwania nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia.
Sasa macho yote yanaelekezwa kwenye nusu fainali, ambapo wachezaji wa Tanzania wanatarajiwa kuonesha tena ubora na ari ya ushindani, wakilenga kufanikisha ndoto ya taifa ya kushiriki michuano ya dunia.
The post Kriketi yaelekeza nguvu nusu fainali first appeared on SpotiLEO.