Klabu ya Simba SC imemtolea shukrani za dhati Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuiongoza timu hiyo katika mchezo muhimu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United.
Kocha Morocco, ambaye ni Kocha Mkuu wa Taifa Stars, alijiunga na kikosi cha Simba kwa ruhusa maalum kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kufanikiwa kukiongoza timu hiyo kupata ushindi muhimu uliowavusha hatua ya awali ya michuano hiyo.
“Shukrani za dhati kwa Kocha Hemed Suleiman ‘Morocco’ kwa kuongoza kikosi chetu katika mchezo muhimu wa jana wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, na kufanikiwa kutuvusha”.
“Shukrani pia kwa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kwa kumruhusu Kocha Morocco ambaye ni Kocha wa Taifa Stars kujiunga nasi,” ilisomeka taarifa ya Simba SC kwenye ukurasa wao wa Instagram.