
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasalimia na kuzungumza na Wananchi wa Ilala-Machinga Complex leo Oktoba 01, 2025 akiendelea na mikutano yake ya kampeni kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mara baada ya kuwasalimia Wananchi hao,Dkt.Nchimbi pia alipata nafasi ya kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ilala Ndugu Mussa Azzan Zungu pamoja na Madiwani .
Pamoja na hayo Dkt.Nchimbi amewahamiza Wananchi hao kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29,2025 na kumpigia kura za kutosha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Dkt.Samia Suluhu Hassan,Wabunge na Mdiwani na hatimae kuibuka na ushindi wa Kishindo.
Dkt. Nchimbi anahitimisha kampeni zake leo kwa mkoa wa Dar es Salaam akifikisha mkoa wa 15 tangu kuzinduliwa kwa kampeni hizo Agosti 28,2025 jijini Dar na kuelekea mikoa mingine kusaka kura za ushindi wa kishindo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).