WAKIWA kwenye hesabu za kumtafuta kocha mpya, Msimbazi wataendelea kukosa huduma ya wachezaji wawili kwenye mchezo wa leo Oktoba Mosi 2025 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Namungo.
Simba SC kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi Suleman Matola ambaye atakiongoza kikosi hicho kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC.
Katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United, Simba SC ilikuwa chini ya Kocha Mkuu Hemed Morocco ambaye alikuwa hapo kwa muda maalumu kwa mchezo huo.
Hayo yote yalitokana na Fadlu Davids ambaye alikuwa na timu nchini Misri kwenye kambi kupata dili katika timu nyingine ambayo ni Raja Casablanca ya Morocoo.
Kuelekea kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Mkapa wachezaji wawili wa Simba SC hawapo kwenye mpango wa mchezo ambao ni Abdoulazack Hamza na kiungo mshambuliaji, Mohamed Bajaber kutokana na majeraha.
Bajaber tangu amejiunga na Simba msimu huu akitokea Polisi Kenya, hakufanikiwa kucheza mchezo wowote wa mashindano kutokana na majeraha ya nyama za paja aliyoyapata kambini nchini Misri.
Kwa mujibu wa kocha msaidizi wat imu hiyo, Selemani Matola nyota hao hawatakuwepo katika mipango yake ya mchezo wa kesho kutokana na majeraha, hivi sasa wanaendelea na matibabu kuhakikisha wanarejea haraka.