Kwenye kikao cha kumfukuza Kocha Foili kilichofanyika jana Mbeya kwenye Hoteli iliyopo Mafiati
Kocha kauliza mnanifukuza kwani mimi ndio nimesajili Wastaafu? Wakajibu hapana, akauliza tena mimi ndio nimesajili Streka mechi tatu no on target ? Wakasema hapana
Akauliza tena sasa mimi kosa langu nini? Wakamwambia Mashabiki hawakutaki jiuzulu, akawambia mimi sijaajiriwa na mashabiki nifukuzeni nyie
Sasa ngondo ni kwamba hawataki kumfukuza maana hawawezi kulipa gharama za kuvunja mkataba na Foili hataki kujiuzulu maana atakosa mpunga wake
Sasa wanaishi pamoja lakini hawapendani
Anaandika Ahmed Ally Msemaji wa Klabu ya Simba