Uongozi wa Klabu ya Coastal Union umetangaza rasmi kufikia makubaliano ya pande zote mbili kusitisha kandarasi ya Kocha Mkuu, Ali Mohammed Ameir.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imemshukuru Ameir kwa mchango na huduma yake kwa kipindi chote ambacho aliiongoza timu, ikisisitiza mchango wake kuwa wa thamani kubwa katika maendeleo ya kikosi hicho.
Coastal Union wameweka wazi kuwa watatoa taarifa kwa umma hivi karibuni kuhusu mabadiliko na muundo mpya wa benchi la ufundi muda mchache ujao.