Mwanahabari wa michezo, @abdulmkeyenge1, amemtolea povu mchezaji Elie Mpanzu Kibisawala, akimtaka kurejea katika ubora wake wa awali na kucheza kama staa halisi wa timu.
“Mpanzu Kibisawala ajifunze kucheza kama staa wa timu. Staa wa timu hachezi anavyocheza yeye. Anacheza kwa kumiminika jasho na kuwanyima raha wapinzani muda mwingi sio kutolewa kama ilivyo kwake. Now days ameanza kuwa mchezaji wa kawaida. Ni kawaida mno, lakini watu wanajua quality kubwa iliyoko miguuni mwake. Huyu sio yeye. Arudi nyuma na kuzitazama video zake atajua nini Simba inataka kutoka kwake.” Alisema @abdulmkeyenge1