LONDON: NYOTA wa real madrid Jude Bellingham ameshindwa kurejea katika kikosi cha England licha ya kurejea uwanjani na Real Madrid baada ya kupona jeraha, huku kocha mkuu ‘the three lions’ Thomas Tuchel akisisitiza kuwa hakuna mchezaji mwenye “hakikisho” la nafasi katika timu yake.
Tuchel ameamua kubaki na kikosi kilekile kilichompa ushindi wa kufuzu Kombe la Dunia mwezi uliopita dhidi ya Andorra na Serbia, akieleza kuwa wachezaji hao walikuwa na kiiwango kizuri hususan kwenye ushindi wa mabao 5-0 mjini Belgrade na hivyo wanastahili kupewa nafasi nyingine.
Uamuzi huo umemuacha nje kiungo Bellingham, ambaye amerejea kwa Real Madrid na kucheza mechi nne mfululizo baada ya kuwa nje kwa miezi miwili kufuatia upasuaji wa bega. Pia, Phil Foden wa Manchester City hakujumuishwa licha ya kuonesha kiwango bora hivi karibuni.
Kutokuwepo kwa Bellingham kumezua mjadala zaidi kutokana na mchango wake mkubwa kwa timu ya taifa. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 22 alipigiwa kura na mashabiki Jumatano kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa England kwa msimu wa 2024/25, baada ya kuibuka shujaa katika fainali za Euro mwaka jana ikiwemo bao la kusawazisha dakika za lala salama dhidi ya Slovakia katika hatua ya 16 bora.
Zaidi, mnamo Agosti Tuchel aliomba radhi hadharani kwa Bellingham baada ya kauli yake iliyozua gumzo kwamba tabia ya mchezaji huyo “inaweza kuchukiza,” akisisitiza kuwa hakukuwa na ajenda ya siri wala binafsi katika maneno yake.
The post Bellingham atachwa tena England first appeared on SpotiLEO.