Wakati tetesi za aliyekuwa kocha wa Gaborone United raia wa Bulgaria Dimitar Nikolaev Pantev kujiunga na wekundu wa Msimbazi kuwa kocha mkuu mpya wa klabu hiyo upande wa pili kwa Mabingwa wa Tanzania tetesi za kuachana na kocha wao Romain Folz zimeshika kasi.
Taarifa hizo zinazohusisha wababe wa soka la Tanzania kama zikiwa za kweli basi makocha hao watapishana mmoja akiondoka kwenye klabu yenye makao makuu mitaa ya Jangwani huku mwingine akijiunga na klabu yake ya mitaa ya Msimbazi.