“Tangu niwe kocha, sijawahi kukutana na mpinzani mgumu kumkabili kama Young Africans.. Kiukwelil naipenda Tanzania ni Nchi nzuri yenye kila aina ya maisha, nitaïkumbuka Daima lakini pia ile Young Africans sitokuja kuisahau”
“Aaaa. Mechi ambayo nilichanganyikiwa sikujua nini cha kufanya, ni ile ya Ngao ya jami waliyo tufunga goli moja. Goll la Maxi Mpia. Ni namna walivyo anza kulitengeneza golilile. Zilipigwa pasi zaidi ya kumi na tisa. llifika hatua mpaka nikawa najiuliza hawa wapinzani wetu huwa wanatumia nini kuwafundisha wachezaji wao? Maana walikuwa fiti kila engo.
Pumzi, kasi na maarifa makubwa. Lile soka la Kaskazini ndilo ambalo walikuwa nalo. Nashukuru Mungu wachezaji wangu niliwapa mbinu ya kukabillana nao hasa nikiwaambia wasishindane nao. Tucheze soka letu, ile ilikuwa mbinu ya kupunguza idadi kubwa ya magoli”
“Natamani siku nilipize kisasi nikiwa hapa Raja Casablanca”
Voice 🗣 FADLU DAVIS aliyekuwa kocha wa simba kwenye mahijiano na kipindi cha speak time huko misri