Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe amefunguka muda mfupi baada ya aliyekuwa Skauti Mkuu wa Simba kutangaza kujiuzulu nafasi yake.
Ally Kamwe ameandika ujumbe unaohusishwa kuwa unawalenga watani zao Simba akisisitiza kuwa taarifa alizozipata kupata kwa jasusi wao ni kuwa muda wowote taarifa ya CEO kujiuzulu itatoka.
“Jasusi wetu Hana Bayaaa.. Jana alisema Kuna Kikao na Leo watu wameanza kujiuzulu mmoja mmoja”
“Muda wowote Taarifa ya CEO kujiuzulu itatoka .. Wanajaribu kumshauri asiondoke Lakini mpaka asubuhi ya Leo, Bi Dada kashikilia msimamo wake”
“Hoja ya Dada ni kupelekwa pelekwa kama Ng’ombe bila kushirikishwa.. Viongozi wa Juu wanafanya maamuzi ya Hovyo na ya aibu kwa Klabu, halafu Yeye anapewa lawama. HATAKI TENA” Ameandika Ally Kamwe.