Klabu ya Simba Sc imemtambulisha kocha Dimitri Pantev kama meneja wa timu hiyo huku vyanzo vikieleza kocha mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi atakuwa Selemani Matola kwenye makaratasi ingawa Pandev atakuwa kiongozi na mtendaji mbele ya benchi la ufundi wakati wa michezo.
Kocha huyo raia wa Bulgaria ana leseni ya UEFA A hivyo hana vigezo ya kusimama kama Kocha Mkuu kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwa anatakiwa kuwa na leseni za CAF A au CAF Pro Licence au UEFA Pro Licence kwa Kocha anayetumia leseni kutoka Mashirikisho mengine nje na CAF.
Hali hii ilishawahi kutokea huko Azam Fc wakati Yousuf Dabo ambaye alikuwa anatambulika kama Kocha Mkuu alikosa leseni stahiki hivyo Azam Fc wakamteua Bruno Ferry Kocha Mkuu kwenye makaratasi huku Dabo ambaye alitajwa kama Kocha Msaidizi akionekana kama ndiye Kocha kiongozi na mtendaji mbele ya benchi la ufundi wakati wa michezo.
Hata hivyo, taarifa ya Simba Sc imemtambulisha Pantev kama Meneja wa timu hiyo huku sintofahamu ikizuka juu ya nani hasa atakuwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo na ni ipi nafasi ya ya Selemani Matola ambaye awali alitambulishwa kama Kocha wa muda (caretaker) baada ya kuondoka kwa Fadlu Davids?