Yanga tayari imeachana rasmi na kocha wao mkuu Romain Folz na utaratibu wa kutafuta kocha mpya upo ukingoni
Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya kikosi hicho zinaeleza kwamba kabla ya kumalizika wiki ijayo tayari watakuwa washamtangaza kocha mpya wa kikosi hicho
Romain Folz kwa sasa amerejea Afrika Kusini na Yangasc muda wowote kuanzia hivi sasa watatoa taarifa rasmi kwa umma.