DAR ES SALAAM:MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Isihaka Nassoro, maarufu kama Aslay, amesema kwa sasa hana mpango wa kuingia katika mahusiano mapya ya kimapenzi kutokana na changamoto alizopitia huko nyuma.
Aslay amesema anachukua muda kujitafakari kabla ya kuingia tena kwenye uhusiano wa kimapenzi ili kuepuka maumivu aliyoyapata awali.
“Nilishawahi kuumia kwenye mahusiano ya kimapenzi, lakini mahusiano hayo hayakuwa kati yangu na mama mtoto wangu, Tessy, bali ni ya mwanamke mwingine. Ndio maana kwa sasa nipo single,” amesema Aslay.
Msanii huyo ambaye ana mtoto mmoja na Tessy, ameongeza kuwa sababu kubwa ya kutokuwa na mpenzi kwa sasa ni hofu ya kurudia makosa ya zamani.
“Sitaki kukurupuka kutafuta mahusiano mapya kwa sababu wanawake wengine wanakupenda kwa kuwa wewe ni msanii, na wengine wanakuwa na tamaa tu,” ameongeza.
Aslay amesisitiza kuwa kwa sasa amejikita zaidi katika kazi yake ya muziki na malezi ya mtoto wake, huku akisema muda ukifika wa kuwa kwenye mahusiano mapya, ataweka wazi kwa mashabiki wake.
The post Aslay afunguka sababu za kuendelea kuwa single baada ya kuachana na Tessy first appeared on SpotiLEO.