MENEJA mpya wa Simba, Dimitar Pantev, jana Jumatatu alianza kazi ya kukinoa kikosi hicho, huku akiweka bayana kuridhishwa na ubora wa wachezaji aliowakuta baada ya kufanya tathmini ya awali akisema wanaweza kufikia malengo msimu huu.
Moja ya malengo ya Simba msimu huu ni kuhakikisha inarejesha mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (FA) ambayo inayasotea kwa misimu minne mfululizo pamoja na kufika mbali katika michuano ya CAF ikiwa ipo raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Nilichokiona kwa wachezaji mmoja mmoja katika tathimini yangu kimenipa matumaini. Hii ni timu yenye vipaji vikubwa, kila mmoja ana kitu cha tofauti. Kazi yangu ni kuhakikisha tunatengeneza mfumo wa pamoja unaojumuisha uwezo wa kila mmoja,” alisema Dimitar aliyewahi kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Cameroon na Botswana akiwa na timu za Victory United na
Tofauti na Fadlu Davids ambaye mara nyingi alipendelea kutumia mfumo wa 4-2-3-1 ambao umekuwa ukilenga uwepo wa uwiano katika kulinda na kushambulia kutokana na kuwa na viungo wawili wenye uwezo mkubwa zaidi wa kulinda, Dimitar ni muumini mkubwa wa mfumo wa 4-3-3.
“Tutaona namna bora zaidi ambayo inaweza kutufanya kuwa bora kama timu uwanjani, tutaenda hatua kwa hatua, naamini inawezekana na ndio maana nipo hapa,” alisema kocha huyo