Siku ya Jana kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya vyombo vya habari kusambaza Maneno kuwa Mchezaji wa zamani wa Simba Fabrice Ngoma kuwa amesema Wachezaji wazawa wa Tanzania ni wachawi huku kwenye taarifa hiyo ikiwataja baadhi ya nyota aliokuwa akikipoga nao kwenye klabu Moja
Nyota huyo Raia wa Congo DR amekanusha taarifa hizo akieleza kuwa hajazungumza Maneno hayo mahali popote Aidha amewalalamikia baadhi ya waandishi wa habari ambao wamesambaza taarifa hizo akiwataka kuwaheshimu wachezaji kwani nje ya Mpira ni familia na ni Wazazi
Aidha Ngoma ameiomba Serikali ya Tanzania kuwafungia waandishi wa habari ambao wameshindwa kufuata weledi wa kazi Yao
Ngoma ameandika hayo kwenye chapisho la ukurasa wa Sportsbetyanzania ambao walichapisha kauli hiyo ya Ngoma kuwa amesema Wachezaji wazawa wa Tanzania ni wachawi.
Ngoma ameandika ✍🏿
“why the journalist from Tanzania doesn’t respect you, the player, really we are parents of a family, we must respect us, it’s really important, the leaders of Tanzania, we must ban the journalist, they are not at school, it’s really regrettable”
Kwa Tafsiri ya Kiswahili
“Mbona mwandishi wa Tanzania haujiheshimu, Wachezaji sisi ni wazazi wa familia lazima tuheshimiane ni muhimu viongozi wa tanzania wapige marufuku wanahabari wasio na shule inasikitisha sana.